Israel yakaa shingo ngumu Gaza

Dismas Otuke
1 Min Read
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amekataa abadan kusitisha mashambulizi katika ukanda wa Gaza licha shinikizo kutoka kwa washirika wa karibu Marekani.

Netanyahu alinukuliwa akisema kamwe hatashurututishwa, punde baada ya mazungumzo ya simu kwa dakika 40 na Rais wa Marekani Joe Bidden.

Waziri huyo Mkuu amesimama kidete kuwa kamwe hatatambua taifa Palestina na kufanya hivyo ni kutangaza ushindi wa wanamgambo dhidi ya Israel.

Haya yanajiri huku majeshi ya Israel yakiendeleza mashambulizi katika ukanda wa Gaza ambapo Wapalestina 28,663, wameuawa na wengine 68,395 kujeruhiwa tangu kuanza kwa makabiliano kati ya Israel na wanamgambo wa Hezbollah Oktoba 7 mwaka uiliopta.

Website |  + posts
Share This Article