Israel yadai kumuua kamanda wa jeshi la majini la Iran IRGC

Martin Mwanje
1 Min Read
Picha kwa hisani ya TASNIM

Israel imedai imemuua kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC), Alireza Tangsiri.

Waziri wa Ulinzi wa Israel, Israel Katz, amesema Tangsiri alikuwa “anahusika moja kwa moja na kitendo cha kigaidi cha kushambulia na kufunga Mlango wa Hormuz,” na kwamba “ameuawa kwa shambulio.”

Ameongeza kuwa maafisa wengine kadhaa waandamizi wa jeshi la majini pia wameuawa.

Hadi sasa, Iran haijatoa tamko lolote kuhusu taarifa hiyo.

Taarifa ya BBC

Share This Article