Iran imekana madai kwamba ilihusika katika utekelezaji wa mashambulizi ya droni huko Jordan ambayo yalisababisha vifo vya raia watatu wa Marekani na wengine kadhaa wakajeruhiwa.
Rais wa Marekani Joe Biden na waziri wa mambo ya nje Uingereza David Cameron wamelaumu makundi yanayoungwa mkono na Iran kwa mashambulizi hayo ya Jumapili karibu na mpaka wa Syria.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje nchini Iran Nasser Kanaani anasema kwamba makundi hayo yanajibu tu ukatili wa utawala na kamwe hayapokei maagizo kutoka kwa Iran.
“Makundi haya yanachukua hatua kulingana na kanuni zao na mambo wanayochukulia kuwa muhimu pamoja na maslahi ya nchi zao na watu wao.” alisema Kanaani.
Wawakilishi wa taifa la Iran katika umoja wa mataifa pia walisema kupitia taarifa kwamba Iran haihusiki kamwe na mashambulizi hayo wakisema yalichochewa na uhasama kati ya wanajeshi wa Marekani na makundi ya waasi katika eneo hilo.
Wakati huo huo muungano wa kiisilamu wa maasi nchini Iraq, an umbrella ambalo ni shirika la makundi yaliyojihami yanayoungwa mkono na Iraq umekiri kutekeleza shambulizi hilo.
Mashambulizi ya ndege zisizoendeshwa na marubani au ukipenda droni dhidi ya kituo cha “Tower 22” yalisababisha kifo cha kwanza cha raia wa Marekani kupitia kwa mashambulizi ya adui tangu vita vya Gaza vilipoanza.