Balozi wa Iran nchini Kenya Dkt. Jafar Barmaki, ameelezea nia ya nchi yake kuwekeza katika sekta ya uzalishaji wa bidhaa na teknohama katika kauti ya Siaya.
Dkt. Jafar aliyemtembelea Gavana wa Siaya James Orengo siku ya Ijumaa, alitoa wito kwa serikali ya kaunti hiyo kutambua maeneo wangependa kushirikiana na serikali ya Iran, ili kufanikisha katika muda mfupi iwezekanavyo.
“Huenda sijwaletea fedha lakini ninaweza waletea biashara, na hiyo itakuwa na manufaa kuliko fedha huku pande zote mbili zikinufaika,” alisema balozi huyo.
Miongoni mwa maeneo muhimu yaloyoangaziwa katika mkutano huo ni pamoja na kilimo, elimu na teknohama.
Aidha Dkt. Jafar alisema serikali ya Iran iko tayari kutoa msaada wa vifaa vya matibabu katika hospitali za kaunti hiyo hata kwa mkopo baada ya serikali hizo mbili kukubaliana.
Gavana wa Orengo aliagiza kuwa kaunti hiyo inapaswa kuwavutia wawekezaji kutoka kwa sekta za umma na kibinafsi kutoka Iran.