IPOA yatakiwa kuhakikisha uwazi na uwajibikaji katika idara ya polisi

Martin Mwanje
1 Min Read
Dkt. Raymond Omollo - Katibu katika Wizara ya Usalama wa Taifa

Mamlaka ya Kuangazia Utenda Kazi katika Idara ya Polisi (IPOA) imetakiwa kutoa kipaumbele kwa haki za binadamu, uwajibikaji na uwazi ulioboreshwa katika idara ya polisi. 

Hayo yamesemwa na Katibu katika Wizara ya Usalama wa Taifa Dkt. Raymond Omollo wakati akizindua warsha ya utoaji mafunzo ya siku tano kwa maafisa wapya wa mamlaka hiyo iliyoanza leo Jumatatu mjini Naivasha.

Amesisitiza umuhimu kuimarisha wajibu wa IPOA katika kuhamasisha uwajibikaji, uwazi na haki za binadamu katika idara ya polisi.

Aidha, Dkt. Omollo ameelezea dhamira ya serikali kukuza mtazamo unaoheshimu haki za binadamu katika utekelezaji wa sheria, akiitaja IPOA kuwa daraja muhimu linalouwaunganisha polisi na umma.

“Katika muktadha wa polisi na haki za binadamu, Kenya imepiga hatua kubwa katika kuangazia uhusiano kati ya utekelezaji wa sheria na kuheshimu haki za binadamu,” alisema Dkt. Omollo.

“Muhimu miongoni mwa hatua hizo ni utekelezaji wa mipangokazi thabiti ya kisheria na kitaasisi ili kuhamasisha uwazi, uwajibikaji na uaminifu katika mifumo yetu ya utekelezaji wa sheria.”

Mwenyekiti mpya wa IPOA Isaak Hassan mamlaka hiyo itatekeleza kikamilifu marekebisho katika idara ya polisi kama ilivyopendekezwa na jopokazi lililoongozwa na Jaji Mkuu Mstaafu David Maraga.

 

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *