Kamati ya kimataifa ya Olimpiki IOC imeridhishwa na hatua za miradi ya kuimarisha ukuzaji vipaji iliyowekwa na Kamati ya Olimpiki nchini NOCK kwa usaidizi wa serikali.
Haya yamesemwa na Rais wa kamati ya kimataifa ya Olimpiki IOC Thomas Bach, alipofanya kikao na wanahabari Jumamosi jioni katika kaunti ya Nairobi.
Bach amepongeza hatua zilizopigwa na shirika la kukabiliana na ulaji muku nchini ADAK ,katika juhudi za kupunguza visa vya ulaji muk,u akiirai serikali kuendelea kufadhili mipango hiyo.
Bach ambaye amekuwa kwenye ziara ya siku tatu nchini alikamilisha ziara yake Jumamosi baada ya kutembelea kambi ya wanariadha wakimbizi ya Kakuma kaunti ya Turkana.
Kinara huyo wa IOC alitoa ahadi ya kupiga Kenya jeki kwa maandalizi yake kwa michezo ya Olimpiki ya vijana mwaka 2026 mjini Dakar Senegal, na pia Michezo ya Olimpiki ya mjini Los Angeles Marekani mwaka 2028.