Ingebrigtsen avunja rekodi za Dunia mita 1500 ukumbini na maili moja

Dismas Otuke
1 Min Read

Yakub Ingebrgsten wa Norway alivunja rekodi mbili za dunia jana usiku katika mashindano ya World Indoor Meeting, yaliyoandaliwa mjini Lievin nchini Ufaransa.

Mshindi huyo wa dhahabu mbili za Olimpiki alivunja rekodi ya dunia ya mita 15000 ya mbio za ukumbini, akiweka rekodi mpya ya dunia ya dakika 3 sekunde 29.63, akivunja rekodi yake ya mwaka 2022.

Ingebrigsten pia alivunja rekodi ya mbio za maili moja, akiziparakasa kwa muda wa dakika 3 sekunde 45.14, akivunja rekodi iliyowekwa wiki jana na Yared Nuguse wa Marekani ya dakika 3 sekunde 46.63.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *