India yawania maandalizi ya Michezo ya Olimpiki mwaka 2036

Dismas Otuke
1 Min Read

India imetangaza kuwania maandalizi ya michezo ya Olimpiki ya mwaka 2036 ikishindana na Poland na Indonesia.

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi amethibitisha utashi wa taifa hilo lenye idadi kubwa ya watu duniani likiwa na watu bilioni 1.4 kuandaa Michezo hiyo ya Olimpiki ya mwaka 2036 pamoja na ile ya Olimpiki kwa walemavu.

Huenda uwanja mkubwa zaidi ulimwenguni wa Narendra Modi unaomudu watu 132,000 ukatumika kuandaa mkchezo hiyo endapo India itafanikiwa kutwikwa jukumu la michezo ya Olimpiki.

Mataifa mengine yaliyodhihirisha utashi wa kuandaa michezo hiyo ya mwaka 2036 ni pamoja na Indonesia na Poland.

Website |  + posts
Share This Article