Imani ya Wakenya kwa Kipyegon na Wanyonyi kutwaa dhahabu Mashindano ya Riadha ya Dunia

Dismas Otuke
2 Min Read

Bingwa mara tatu wa dunia katika mbio za mita 1500 faith Kipyegon na Emanuel Wanyonyi wanaangaziwa na Wakenya zaidi ya milioni 40 kunyakua dhahabu kwenye fainali za mbio za mita 5,000 na mita 800, katika siku ya  nane ya mashindano ya Riadha Duniani mjini budapest Jumamosi usiku.

Wanyonyi aliye na umri wa miaka 19 na ambaye pia ni bingwa wa dunia kwa chipukizi walio chini ya umri wa miaka 20 atakuwa akishiriki fainali ya Jumamosi kwa mara ya pili mtaliwa na akiwa mkenya pekee baada ya kumaliza wa nne mwaka uliopita.

Wanyonyi ambaye pia ameshinda mbio mbili za Diamond League msimu huu atakabiliana na upinzani kutoka kwa Marco Arop wa Canada,Tshepiso MASALELA wa Botswana,Bryce HOPPEL wa Marekani,Ben Pattison wa Uingereza na Djamel SEDJATI na Slimane MOULA wote kutoka Algeria.

Emmanuel Wanyonyi wa  Kenya akitimka nusu fainali ya mashindano ya dunia mjini Budapest

Fainali hiyo itang’oa nanga saa tatu unusu usiku .

Mshikilizi wa rekodi ya dunia Faith Kipyegobn atawaongoza bingwa wa jumuiya ya madola Beatrice Chebet na Lillian Kasait katika fainali ya mita 5,000 kuanzia saa nne kasoro dakika 10 usiku.

Upinzani mkali kwa Wakenya unatarajiwa kutoka kwa Siffan Hassan wa Uholanzi,na Waethiopia Ejgayehu TAYE na Freweyni HAILU.

Vivian Cheruiyot alitwaa dhahabu ya mbio hizo mara mbili mwaka 2009 na mwaka 2011 kabla ya Hellen Obiri kushinda mataji mawili mwaka 2017 na 2019.

Share This Article