Ilani ya kunadi mali ya Tuju yatolewa

Tom Mathinji
2 Min Read
Raphael Tuju.

Aliyekuwa waziri katika serikali ya Jubilee Raphael Tuju, amepokea ilani ya siku 45 ya kulipa shilingi bilioni 4.5 anazodaiwa na benki moja, au mali yake iliyoko katika mtaa wa Karen, Jijini Nairobi inadiwe.

Katika barua iliyoandikwa Julai 24, 2024 kampuni ya kunadi mali ya Garam Investments, ilisema imepokea maagizo kutoka kwa wakili  Kaplan and Stratton advocates kwa niaba ya benki ya maendeleo ya kanda ya Afrika Mashariki (EADB), kuuza mali kwa jina  Dari Business Park na Entim Sidai Wellness Sanctuary properties, Oktoba 1, 2024 iwapo waziri huyo wa zamani hatalipa shilingi bilioni 4.5 anazodaiwa.

Ilani hiyo ya kunadi mali ya Tuju, inajiri baada ya mzozo wa muda mrefu Mahakamani kati ya waziri huyo wa zamani na benki hiyo kuhusu dola Milioni 9.3 ambazo Tuju alichukua kama mkopo mwaka 2015, ili kufadhili ujenzi wa nyumba za kuuza Jijini Nairobi, ambazo bado hajalipa.

Swala hilo limekuwa mahakamani kuanzia nchini Uingereza, mahakama kuu na mahakama ya rufaa hapa nchini Kenya, na sasa katika Mahakama ya upeo, huku mahakama hizo zikimuagiza Tuju kulipa deni hilo.

Huku ikitupilia mbali rufaa iliyowasilishwa na Tuju, Majaji wa Mahakama ya rufaa waliokuwa wakisikiliza kesi hiyo walisema;” Mlalamishi anatumia mbinu kususia kutekeleza wajibu wake kuambatana na kandarasi,”.

TAGGED:
Share This Article