IGAD kusaidia Mataifa wanachama kukabiliana na majanga

Tom Mathinji
1 Min Read
Maporomoko ya ardhi yakumba kusini mwa Ethiopia.

Shririka la IGAD, limeelezea kujitolea kwake kusaidia mataifa wanachama kukabiliana na majanga na pia kuzuia majanga hayo katika siku zijazo.

Kupitia kwa taarifa, Katibu Mkuu wa IGAD Dkt. Workneh Gebeyehu, alituma rambairambi zake kwa familia zilizoathiriwa na maporomoko ya ardhi kusini mwa Ethiopia, huku akiwataka raia kufuata taratibu za kiusalama ili kulinda maisha.

“Tutaendelea kushuhudia majanga kutokana na mabadiliko ya tabia nchi, tunahimiza kila mmoja kufuata taratibu za kiusalama ili kuokoa maisha na kuzuia majanga zaidi,” alisema Workneh.

Matamshi yake yanajiri baada ya maporomoko ya ardhi kushuhudiwa siku ya Jumapili jioni na Jumatatu asubuhi baada ya mvua kubwa kukumba eneo la Gofa kusini mwa Ethiopia.

Hadi kufikia sasa makundi ya uokoaji yamepata miili 229 ya watu waliofariki katika mikasa huyo miwili, kusini mwa Ethiopia.

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *