IGAD kufanya mkutano kwa njia ya mtandao kujadili mgogoro wa Sudan Kusini

CGTN Kiswahili
1 Min Read
Watu wakikimbia machafuko nchini Sudan Kusini / Picha kwa hisani ya "The Independent"

Shirika la Maendeleo la Serikali za Nchi za Afrika Mashariki (IGAD) linatarajia kufanya mkutano wake wa 43 wa Wakuu wa Nchi na Serikali leo Jumatano kwa njia ya mtandao ili kujadili hali inayobadilika nchini Sudan Kusini kufuatia mgogoro wa kiusalama nchini humo.

Katika taarifa yake, IGAD imesema imeshikilia ahadi yake ya kutumia mazungumzo, kupunguza mvutano, na kutafuta hatima ya amani kwa watu wa Sudan Kusini.

Mapigano makali yameibuka katikati ya mwezi Februari kati ya Jeshi la Sudan Kusini na makundi ya kiraia yenye silaha katika kaunti ya Nasir nchini humo, na mvutano kuongezeka baada ya serikali kutangaza mpango wa kupeleka vikosi vipya katika kaunti hiyo kuchukua nafasi ya vikosi vilivyokuwepo kwa miaka mingi katika kaunti hiyo.

Wiki iliyopita, Katibu Mkuu wa IGAD Workneh Gebeyehu alitoa wito wa kujizuia na mazungumzo ili kupunguza mvutano unaoongezeka nchini Sudan Kusini.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *