Siku kuu ya Idd-Ul-Fitr, itaadhimishwa Jumapili tarehe 30 mwezi Machi kote duniani kufuatia kuonekana kwa mwandamo wa mwezi Jumamosi jioni.
Hii ina maana kuwa Waislamu walifunga kwa siku 29 katika kalenda yao ya Ramadhan mwaka, ambapo mfungo huwa aidha siku 29 au 30.
Desturi Waislamu wataandaa ibada za maombi katika misikiti kabla ya kusherehekea Idd pamoja na ndugu, jamii na rafiki na kuwakumbuka pia wasiobahatika katika jamii kwa kutoa misaada.
Mfungo wa Ramadhan ni mojawapo wa nguzo tano kuu za dini ya Kiislamu.
Mfungo huu unatoa fursa kwa Waislamu kuimarisha imani yao, kujitafakari, na kuungana na jamii zao katika hali ya upendo na mshikamano.
Aidha, ni wakati wa kuonyesha shukrani kwa baraka wanazopokea huku wakijitahidi kusaidia wale wenye uhitaji kwa njia mbalimbali.