Idadi ya waliopiga kura mapema Marekani yapita milioni 81

Martin Mwanje
1 Min Read

Idadi ya waliopiga kura mapema nchini Marekani imepita milioni 81, kulingana na Chuo Kikuu cha Florida Election Lab.

Hadi mkesha wa kuamkia siku ya kupiga kura, watu 81,379,684, tayari walikuwa wameshapiga kura, 44,402,375 wakiwa wamefika katika vituo vya kupiga kura wenyewe huku kura 36,977,311 zikiwa zimepigwa kama barua kupitia njia ya posta.

Kuna jambo moja tunaloweza kusema kwa hakika: Desturi za kupiga kura za raia wa Marekani zimebadilika tangu kutokea kwa mlipuko wa Covid.

Ingawa idadi ya wapiga kura wa mapema mwaka huu haitapita ile ya wakati wa janga la Covid, imezidi ile jumla ya kura za mapema zilizopigwa mwaka wa 2016 (milioni 47.2) au 2012 (milioni 46.2).

Ingawa kila jimbo hushughulikia upigaji kura wa mapema kwa njia tofauti na mengi yanazingatiwa.

Hata hivyo, maoni mengi kuhusu upigaji kura wa mapema yanatolewa kulingana na data ya idadi ya watu pekee lakini huwezi kujua ni wagombea kina nani wamepigiwa kura hadi siku ya kuanza kutolewa kwa matokeo.

Share This Article