Idadi ya watu waliofariki kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea katika eneo la Tibet nchini China jana Jumanne asubuhi imefikia 126.
Mamlaka zinasema watu wengine 188 wamejeruhiwa.
Tetemeko hilo lenye ukubwa wa 6.8 katika kipimo cha Richter lilikumba kaunti ya Tingri na kuharibu zaidi ya nyumba 3,600.
Watu wapatao 30,000 hawana makazi.
Maafisa wa zimamoto na wale wa jeshi wameimarisha jitihada za kuwatafuta watu walionaswa chini ya vifusi vya majengo yaliyoanguka.
Hata hivyo, operesheni za kuwatafuta na kuhamisha wakazi zimeripotiwa kukumbwa na changamoto chungu nzima ikiwa ni pamoja na baridi kali zaidi wakati wa usiku.