Huduma ya kitaifa ya Polisi imesema kuwa idadi ya watu waliofariki kutokana na mafuriko nchini imefikia 66.
Idadi hiyo inajumuisha wanaume 50, wanawake wanane na watoto wanane.
Kaunti ya Nairobi ndiyo iliyokuwa na maafa mengi ya mafuriko hato yaliyosababishwa na mvua, ikiwa na 33, ikifuatwa na Mashariki kwa 18 na wanane kutoka bonde la ufa.
Aidha, polisi wameongeza kuwa zaidi ya familia 2,000 zililazimika kuhama makwao kutokana na mafuriko.