Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imetangaza kuwa uchaguzi mdogo wa eneo bunge la Emurua Dikirr utaandaliwa Mei 14 mwaka huu.
IEBC imewataka wote wanaonuia kuwania kiti hicho kuwasilisha karatasi zao kabla au kufikia tarehe 7 mwezi ujao.
Mwenyekiti wa IEBC Erastus Ethekon amemteua Caleb Siriba Gekendo, kuwa msimamizi wa uchaguzi mdogo wa Emurua Dikirr akisaidiwa na Sylvia Jepchumba.
Ethekon ametangaza kuwa tume hiyo inahitaji bajeti ya shilingi milioni 59.38 kuandaa uchaguzi mdogo wa Emurua Dikirr.
Kiti hicho kiliachwa wazi kufuatia kifo cha mbunge Johana Ng’eno kupitia ajali ya ndege Februari 28 mwaka huu.