Idadi ya walioangamia kutokana na tetemeko la ardhi Morocco yapanda hadi 2500

Dismas Otuke
1 Min Read

Zaidi ya watu 2500 wamefariki na wengine takriban 2500, kujeruhiwa vibaya kutokana na tetemeko baya la ardhi lililotokea nchini Morocco kilomita 72 Kusini mashariki mwa mji wa Marrakeshi ulio wa nne kwa ukubwa mapema Jumamosi.

Shughuli za uokoaji zikiingia siku ya tatu.

Serikali imetangaza maombolezo ya kitaifa kote nchini Morocco huku wahisani wakitoa msaada wa damu na chakula kuwaokoa manusura.

Hata hivyo kulingana na maafisa wa shirika la msalaba mwekundu mataumaini ya kuwaokoa waliokwama kwenye vifusi vya majengo yaliyoporomoka yanazidi kudidimia kila siku.

Tetemeko hilo la ardhi ndilo kubwa na baya zaidi kuwahi kushuhudiwa katika taifa hilo la kaskazini mwa Afrika.

Waokoaji pia wanahofia kushuka kwa viwango vya joto nyakati za jioni katika mji wa Marrakesh,  eneo la mkasa huo  inafifisha zaidi matumaini ya kupata majeruhi kwenye vifusi.

Share This Article