Kiongozi wa walio wengi katika bunge la kitaifa ambaye pia ni mbunge wa Kikuyu Kimani Ichungwa, amekanusha madai ya kuwania nafasi ya waziri wa usalama wa ndani baada ya waziri Kithure Kindiki kuidhinishwa na bunge la kitaifa kuwa naibu wa Rais .
Akizungumza katika shule ya msingi ya Pangani eneo bunge la Rabai, kaunti ya Kilifi,mbunge huyo amesema kuwa ameridhishwa na kazi yake bungeni kwa sasa na hana nia ya kujiunga na baraza la Mawaziri.
Akiwa ameandamana na mbunge wa Rabai Kenga Mupe na Kiongozi wa wananwake Kilifi Getrude Mbeyu katika hafla ya kuungua madarasa yaliyojengwa na hazina ya NGCDF na pia kugawa chakula cha msaada,Ichungwa aliongeza kuwa Wabunge walimng’oa mamlakani naibu Rais Rigathi Gachagua kama njia moja ya kukomesha siasa za kikabila.