ICC yamtimua kiongozi wa mashtaka Karim Khan

Mahakama hiyo iliwahakikishia waathiriwa, jamii zilizoathiriwa, mataifa wanachama na makundi ya kijamii kwamba majukumu yake yataendelea bila kukatizwa licha ya mabadiliko ya uongozi.

Tom Mathinji
1 Min Read
Karim Khan.

Mahakama ya kitaifa ya Uhalifu (ICC), imemtimua kiongozi wa mashtaka Karim Khan baada ya uchunguzi wa nchi wanachama kumpata na hati ya ukiukaji wa maadili na utepetevu kwenye majukumu yake.

Kwenye taarifa baada ya uamuzi huo, afisi ya kiongozi wa mashtaka ilikubali maamuzi yaliyoafikiwa kwenye kikao  maalum cha mataifa wanachama wa ICC, kilichomwondoa Khan  afisini.

Afisi hiyo ilithibitisha kuwa manaibu viongozi wa mashtaka Nazhat Shameem Khan na Mame Mandiaye Niang, waendelea kutekeleza majukumu ya afisi hiyo. Wawili hao tayari walikuwa wakitekeleza majukumu ya afisi hiyo baada ya Khan kuondoka afisini mwezi Mei mwaka 2025.

Mahakama hiyo iliwahakikishia waathiriwa, jamii zilizoathiriwa, mataifa wanachama na makundi ya kijamii kwamba majukumu yake yataendelea bila kukatizwa licha ya mabadiliko ya uongozi.

Aidha, mahakama hiyo iliongeza kuwa imejitolea kufanya uchunguzi huru na usioegemea upande wowote chini ya mamlaka ya mahakama hiyo ili kuleta haki kwa waathiriwa.

Karim Asad Ahmad Khan, amehudumu wadhifa wa kiongozi wa mashtaka tangu mwezi Juni mwaka 2021.

TAGGED:
Share This Article