Ian Njoroge, ambaye anadaiwa kumshambulia afisa wa polisi wa trafiki katika barabara ya Kamiti, ameachiliwa na mahakama kwa dhamana ya shilingi 700,000.
Hakimu mkuu mwandamizi wa mahakama ya Milimani Ben Mark Ekhumbi, hakumpa Njoroge fursa ya kuachiliwa huru na pesa taslimu, kutokana na makosa aliyotekeleza.
Njoroge alishtakiwa Jumanne kwa kumjeruhi afisa wa polisi, kukataa kutiwa nguvuni na wizi wa kimabavu, kufuatia tukio lililofanyika siku ya Jumapili.
Vile vile alifikishwa katika mahakama ya trafiki, ambapo alishtakiwa kwa makosa matatu ya kusababisha kizuizi barabarani na kubeba abiria kupita kiasi.
Kulingana na polisi, Njoroge alimwibia afisa wa polisi Jacob Ogendo kifaa cha mawasiliano na simu ya mkononi ya thamani ya shilingi 50,000.