Afisa Mkuu mtendaji wa shirika la Extreme sports Hussein Mohammed amelalama kuhusu kudhilumiwa na kunyanywa na maafisa wa shirikisho la kandanda nchini .
Hussein amesema kuwa alizuiliwa kuingia katika uwanja wa Raila Odinga tarehe 31 mwezi uliopita kwa fainali ya mashindano ya kombe la Gavana wa kaunti ya Homa Bay .
Hussein ameongeza kuwa marefarii waliondolewa na kuizuiliwa kusimamia fainali hiyo.
Ilibidi maafisa wa kaunti kuingilia kati kabla ya mechi kuendelea.
Akizungumza na wanahabari siku ya Ijumaa katika kaunti ya Nairobi, Hussein ambaye ni mmoja wa waaniaji wakuu wa Urais wa FKF katika uchaguzi wa mwezi ujao ,ameshitumu matukio hayo.
Hussein emesema visa kama hivyo vimepitwa na wakati na ni hali ya kurudisha hadhi ya soka nchini.