Huduma za kupachika Figo kupatikana katika hospitali ya chuo Kikuyu Cha Kenyatta

Tom Mathinji
1 Min Read

Hospitali ya rufaa ya chuo kikuu cha Kenyatta inaweka mikakati ya kuzindua huduma za upasuaji wa kupachika figo.

Hatua hiyo inalenga  kuwaokolea wakenya mamilioni ya pesa wanazotumia kugharamia upasuaji huo katika mataifa ya kigeni.

Huduma hiyo itaanza kutolewa baada ya muda wa miezi sita ijayo baada ya kuwekwa kwa vifaa vinavyohitajika kwa upasuaji huo kwenye hospitali hiyo.

Mwenyekiti wa bodi ya hospitali hiyo Olive Mugenda, alisema wasimamizi wa hospitali hiyo waliona haja ya kuzindua huduma hiyo baada ya takwimu kuonyesha kwamba mamia ya wakenya hutafuta huduma hiyo ughaibuni kwa gharama ya juu.

Aliongeza kuwa gharama ya upasuaji huo itashughulikiwa na hazina ya bima ya matibabu ya NHIF ili wakenya waweze kupata huduma hiyo kwa gharama nafuu.

Afisa mkuu wa hospitali hiyo Ahmed Dagane, alisema hospitali hiyo imejitolea kuunga mkono mpango wa serikali wa afya bora kwa wakenya wote.

TAGGED:
Share This Article