HRW: Ushahidi unaonyesha M23 walihusika na mauaji ya DR Congo

Martin Mwanje
2 Min Read
Shule hii ya Kishishe ilitumiwa na M23 kama kambi ya kijeshi

Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch (HRW) linasema limepata ushahidi zaidi kwamba waasi wanaodaiwa kuungwa mkono na Rwanda waliwaua makumi ya watu ambao walizikwa kwenye makaburi ya pamoja mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.

HRW inasema kuwa raia na wanamgambo waliokuwa wametekwa na kundi la waasi la M23 waliuawa katika kijiji cha Kishishe kati ya Novemba mwaka jana na Aprili mwaka huu.

Rwanda imekanusha kuwaunga mkono waasi wa M23 ambao siku za nyuma walisema hawakuhusika na mauaji hayo.

HRW imetoa wito kwa serikali ya Congo kupata usaidizi wa kuchimba makaburi hayo kutoka kwa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika, kurejesha mabaki waliofariki kwa familia na kuwawajibisha waliohusika.

Wapiganaji wa M23 ni akina nani?

Wakijumuisha na wanajeshi wa Congo waliokimbia jeshi, KUchukua silaha kwa mara ya kwanza mwaka 2009 wakiishutumu serikali kwa kuwatenga watutsi walio wachache nchini humo na kushindwa kuheshimu mikataba ya amani ya hapo awali.

Mapema mwaka jana walianza kujipanga upya, muongo mmoja baada ya kupokonywa silaha kama sehemu ya makubaliano ya amani

Waliteka eneo katika jimbo la Kivu Kaskazini na kufanya maelfu ya raia kukimbia makazi yao.

Tangu wakati huo wamejiondoa kutoka kwa baadhi ya maeneo kama sehemu ya mpango wa kikanda wa kusitisha mapigano.

Lakini kundi hilo linasema halitaweka chini silaha hadi serikali ikubali matakwa yake ya kufanya mazungumzo.

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *