Homa Bay Combined watwaa kombe la Eliud Owalo

Dismas Otuke
1 Min Read

Homa Bay Combined waliibwaga Kisumu Combined magoli 4- 2 kupitia mikiki ya penalti na kutawazwa mabingwa wa kombe la Eliud Owalo Super.

Ilibidi mshindi wa mechi hiyo abainike kupitia matuta ya penalti kufuatia sare tasa baada ya dakika 90, katika fainali hiyo ya kusisimua iliyosakatwa katika uga wa Jomo Kenyatta, kaunti ya Kisumu siku ya Alhamisi.

Siaya Combined iliwacharaza Migori Combined mabao 2-1 na kumaliza katika nafasi ya tatu.

Homa Bay walitunukiwa shilingi laki nne huku Kisumu Combined wakipokea shilingi laki tatu.

Mashindano hayo yalifadhiliwa na wakfu wa Waziri Habari, Mawasiliano na Uchumi wa Dijitali Eliud Owalo.

Wachezaji 22 boira walioteuliwa kwenye mashindano hayo watapambana na mabingwa wa ligi kuu Gor Mahia Jumamosi katika uwanja wa Nyilima, eneo bunge la Rarieda kaunti ya Siaya katika pambano la kirafiki.

Share This Article