Mwenyekiti wa kamati ya andalizi ya michuano ya CHAN nchini Kenya, Nicholas Musonye, na Afisa Mkuu Myke Rabar, wameridhishwa na matayarisho ya Tanzania kwa fainali zitakazoandaliwa kati ya Agosti 2 na 30 mwaka huu.
Maafisa hao wawili walizuru uwanja wa kitaifa wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam na kuhudhuria pia utiaji saini wa kuongezwa kwa mkataba kati ya shirikisho la soka Afrika CAF na kampuni ya mafuta ya Ufaransa Total Energies.
Fainali za nane za CHAN ziliratibiwa kuandaliwa kuanzia Februari mosi na mataifa ya Kenya, Tanzania, na Uganda, lakini zikaahirishwa ili kuruhusu kukamilishwa kwa matayarisho.
Kenya imejumuishwa kundi A katika michuano ya CHAN pamoja na Morocco, DR Congo, Zambia, na Angola.