Hofu ya mbolea ya ruzuku yawatafuna wakulima kaskazini mwa Bonde la Ufa

radiotaifa
1 Min Read

Taarifa ya Joseph Mwanjala

Serikali imewahakikishia wakulima katika eneo la kaskazini mwa Bonde la Ufa kuwa hakutashuhudiwa upungufu wa mbolea ili kuwawezesha kushiriki upanzi kwa wakati mwafaka kama njia moja ya kuimarisha uzalishaji na kuafiki usalama wa chakula.

Huku wakulima wakiendelea kujitokeza kwa wingi katika ghala za kitaifa za mazao na nafaka, NCPB mjini Kitale na vituo vingine vya kuuzia mbolea katika kaunti ndogo tano za kaunti hiyo wakati wakiwa hofu ya kukosa bidhaa hiyo, meneja wa NCPB kaskazini mwa Bonde la Ufa Gilbert Rotich amekariri kuwa serikali imejizatiti kuhakikisha mbolea inapatikana kwa wingi.

Rotich amekiri kuwa kumekuwa na changamoto ya usafirishaji wa mbolea hasa inayohitajika na wakulima wa kaunti hiyo kutoka taifa la Morocco na kwamba tatizo hilo limesuluhishwa kwa sasa.

Ameongeza kuwa wameweka mikakati ya kuhakikisha mbolea hiyo inafikishwa katika vituo vyote vya kuuzia mashinani ili kupunguza msongamano katika ghala ya NCPB mjini Kitale.

Haya yanajiri huku wakulima wakitaka serikali kupitia idara ya kilimo  kuwaelimisha kuhusu aina ya mbolea inayoendana na udongo katika  maeneo wanayokuza mimea yao.

Share This Article