Ni afueni kwa idadi kubwa ya wanafunzi wa shule za upili wasiopenda soma la Hisabati, baada ya katibu wa Elimu ya Msingi Dkt. Belio Kipsang kutangaza kuwa somo hilo halitakuwa lazima kwa wanafunzi katika mtaala wa umilisi, CBC.
Kulingana na mabadiliko hayo mapya, wanafunzi wa Gredi ya 9 watalazimishwa kufanya masomo ya Kiingereza, Kiswahili, Elimu ya Viungo vya Mwili (PE) na Mafunzo ya Huduma za Jamii, huku wakichagua masomo mengine yaliyosalia kutoka kwa orodha ya masomo 38, kulingana na taaluma wanazopania kufanya.
Hisabati limekuwa somo la lazima kwa wanafunzi wote katika mtaala uliofutiliwa mbali wa 8-4-4 , pamoja na Kiingereza, Kiswahili, na aidha Kemia, Biolojia, au Fizikia.
Dkt. Kipsang amesema wanafunzi watachagua masomo yao katika muhula wa pili wa Gredi ya 9.