Hezbollah yasema italipiza kisasi dhidi ya Israel baada ya shambulio la vifaa vya mawasiliano

Martin Mwanje
1 Min Read

Kundi la Hezbollah la Lebanon limesema katika taarifa yake siku ya Jumatano kwamba Katibu Mkuu wa kundi hilo, Hassan Nasrallah, atatoa hotuba siku ya Alhamisi, kufuatia milipuko ya vifaa vya mawasiliano kote Lebanon siku ya Jumanne.

Hezbollah imeahidi “kuendeleza operesheni zake za kijeshi dhidi ya Israel kwa kuunga mkono Ukanda wa Gaza” siku moja baada ya milipuko ya vifaa vya mawasiliano vya wanachama wake.

Chama hicho kilisema katika taarifa yake kwamba uungaji mkono kwa Gaza ni tofauti na kile ulichokitaja kuwa ni adhabu kali ijayo kwa adui mhalifu kwa mauaji ya siku ya Jumanne.

Hezbollah inaomboleza vifo vya wapiganaji wake wanane, akiwemo mtoto wa Mbunge wa Hezbollah, Ali Ammar.

Waziri wa Afya wa Lebanon, Firas Al-Abyad alisema idadi ya watu waliojeruhiwa kutokana na milipuko hii ni watu 2,750, pamoja na waliokufa tisa, akiwemo msichana wa miaka minane, akieleza kuwa takwimu hizi si za mwisho bado.

Waziri wa Lebanon alielezea wakati wa mkutano na waandishi wa habari kwamba mejeraha mengi ni mabaya, akibainisha kuwa ni pamoja na majeraha ya uso, mikono, eneo la tumbo na macho, na kuongeza kuwa zaidi ya hospitali 100 nchini Lebanon zinapokea majeruhi.

Share This Article