Hazina ya wanawake kutoa mikopo ya shilingi bilioni 30 ndani ya miaka mitano

Dismas Otuke
1 Min Read

Hazina ya wajasiriamali wanawake inalenga kutoa mikopo ya kima cha shillingi billion 30 kwa wanawake million 5 katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Hazina hiyo Pia inaazimia kutoa mafunzo kwa wanawake milioni moja kuhusu mbinu muhimu za kibiashara, wengine laki mbili kuhusu jinsi ya kupata soko kwa bidhaa zao katika kipindi hicho.

Katibu katika wizara ya jinsia na tende sawazishi Anne Wang’ombe, amesema hazina hiyo itatumia mfumo wa teknolojia ya kisasa ili kuwafikia wanachama zaidi kote nchini.

Zaidi ya shilingi bilioni 27 nukta 8 zimetolewa kwa zaidi ya wanawake milioni mbili kote nchini huku wengine milioni 1 nukta 7 wakipokea mafunzo ya usasiriamali kwa lengo la kuongeza tija.

Website |  + posts
Share This Article