Hatuna budi kuishinda Kenya, asema kocha Pedro Goncalves wa Angola

Angola, maarufu kama Palancas Negras, watakabiliana na Harambee Stars kesho kutwa katika uwanja wa kimataifa wa Kasarani kuanzia saa moja usiku.

Dismas Otuke
1 Min Read

Kocha wa timu ya taifa ya Angola Pedro Gonçalves, ameapa kuishinda Kenya katika mechi ya pili ya kundi A Alhamisi usiku katika uwanja wa kimataifa wa Kasarani.

Akizungumza na Wanahabari, Gonçalves amesema baada ya kupoteza mechi ya ufunguzi dhidi ya Morocco, ni sharti waishinde Harambee Stars ingawa kitakuwa kibarua kigumu.

“Tulicheza vizuri mechi yetu dhidi ya Morocco lakini makosa madogo yalitugharimu, akasema Gonçalves.

Angola, maarufu kama Palancas Negras, watakabiliana na Harambee Stars kesho kutwa katika uwanja wa kimataifa wa Kasarani kuanzia saa moja usiku.

“Mechi yetu ya pili tutakuwa na shinikizo lakini hatuna njia nyingine isipokuwa kuwashinda Kenya,. akasema Gonçalves.

Harambee Stars kwa upande wao watakuwa wakiwinda ushindi wa pili ambao utawaweka katika nafasi nzuri ya kufuzu kwa robo fainali kwa mara ya kwanza.

Tiketi za mechi hiyo itakayosakatwa  kuanzia saa moja usiku zilifungwa kuuzwa leo Jumannne.

Website |  + posts
Share This Article