Hatma ya Rais wa Iran Raeisi haijulikani baada ya ndege yake kuanguka

Dismas Otuke
1 Min Read

Hatma ya Rais wa Iran Ebrahim Raeisi haijulikani, baada ya ndege ya helicopter aliyokuwa ameabiri kuanguka eneo la Jolfa kaskazini mashariki kwa Azerbaijan.

Rais Raeisi alikuwa akirejea baada ya kufungua mradi wa mabwawa ya maji pamoja na mwenzake wa Azerbeijan Ilham Aliyev Jumapili alasiri.

Ndege iliyombebs Rais Raeisi muda mfupi baada ya kupaa Jumapili

Duru za kuaminika zimearifu kuwa ndege hiyo ilikumbwa na hitilafu na kulazimika kutua ghafla kwa nguvu.

Yamkini ndege hiyo ilutua eneo la milimani na ndani ya msitu, kutokana na huenda ilisababishwa na ukungu mkubwa.

Viongozi wa mataifa mbalimbali wameelezea hofu yao kuhusu afya kiongozi huyo.

Ndege hiyo ilikuwa imembeba Rais huyo pamoja na waziri wake wa kigeni.

Raia wengi wa Iran wameonekana wakifurika kwenye misikiti kumwombea kiongozi huyo, huku viongozi wa mataifa mbali mbali wakohofia

Share This Article