Mahakama ya rufaa leo Ijumaa inatarajiwa kuamua kesi iliyowasilishwa na serikali kupinga kusitishwa kwa utekelezaji wa hazina ya bima ya afya ya jamii, SHIF.
Hazina hiyo iliratibiwa kuanza kutekelezwa Januari mosi mwaka huu ambapo kila mfanyakazi angetozwa asilimia 2.75 ya mshahara wake kila mwezi ili kuigharimia.
SHIF inatarajia kuchukua nafasi ya Hazina ya Kitaifa ya Bima ya Afya, NHIF ambayo imekuwepo kwa muda mrefu.