Harusi ya Charlene Ruto na Isaya Yunge kuandaliwa kesho

Itafanyika katika ufukwe wa Hoteli ya Malaika Beach Resort Jijini Mwanza, nchini Tanzania.

Marion Bosire
1 Min Read

Harusi ya binti ya Rais wa Kenya William Ruto, Charlene Ruto na mpenzi wake Isaya Yunge itaandaliwa kesho Novemba 6, 2026 jijini Mwanza nchini Tanzania.

Hafla hiyo itafanyika katika ufukwe wa Hoteli ya Malaika Beach Resort jijini Mwanza, huku maandalizi ya tukio hilo yakianza kushika kasi na kuvuta hisia za watu kutoka pande zote mbili za Afrika Mashariki.

Charlene aliwasili jijini Mwanza nchini jana Jumatano, Novemba 4, 2026 akitumia ndege ya kibinafsi kabla ya kusafirishwa na msafara wa magari ya kifahari hadi hotelini.

Novemba 3, 2026, mrembo huyo aliandaliwa hafla ya kumfunza kabla ya harusi ambapo wahudhuriaji walivaa mavazi ya rangi nyeupe na kahawia.

Rais William Ruto anatarajiwa kuungana na familia katika kusherehekea siku hiyo muhimu kwa binti yake, pamoja na viongozi wengine mashuhuri.

Awali, wapenzi hao walifanya sherehe ya mahari na kuvishana pete za uchumba Agosti 8, 2026 nyumbani kwa Rais William Ruto huko Kilgoris, kaunti ya Narok nchini Kenya.

Sherehe hiyo ya uchumba iliwakutanisha ndugu na jamaa wa pande zote mbili, ikiwa ni sehemu ya taratibu za kimila kabla ya wawili hao kuingia rasmi kwenye ndoa.

Sasa wengi wanaangazia Mwanza, ambako familia hizo mbili zinatarajiwa kuungana katika harusi ya wanao.

Share This Article