Harambee Stars yatua Qatar kwa mechi ya kirafiki

Dismas Otuke
2 Min Read

Timu ya taifa ya soka ya wanaume ya Kenya maarufu kama Harambee Stars imeatua mjini Doha nchini Qatar mapema Jumatano tayari kwa mchuano wa kimataifa wa kirafiki utakaopigwa Alhamisi Septemba 7 .

Kenya chini ya ukufunzi wa kocha Engine Firat inatumia mchuano huo kujiandaa kwa mechi za makundi za kufuzu kwa kombe la dunia hatua ya makundi zinazotazamiwa kuanza mwezi Novemba mwaka huu.

Kikosi cha Harambee Stars kilichosafiri kinawajumuisha wanandinga 26 ambao walipiga kambi ya mazoezi kabla ya ziara yao.

Harambee Stars baadae itachuana na Sudan Kusini katika uwanja wa kimataifa wa Kasarani tarehe 12 mwezi huu katika pambano jingine la kirafiki.

Kenya imejumuishwa kundi F la kufuzu wka kombe al dunia mwaka 2026 pamoja na Ivory Coast,Gambia,Gabon,Burundi na Ushelisheli

Kikosi cha Kenya kilichosafiri kwenda Qatar

Makipa

Ian Otieno (Zesco, Zambia), Byrne Odhiambo (KCB), Patrick Matasi (Kenya Police FC)

Mabeki

Collins Sichenje (AIK, Sweden), Joseph Okumu (Stade Reims, France), Brian Mandela (Mamelodi Sundowns, South Africa), Johnstone Omurwa (Estrela, Portugal), Daniel Anyembe (Viborg, Denmark), Eric Ouma (AIK, Sweden), Amos Nondi (Ararat, Armenia), Abud Omar (Kenya Police).

Viungo

Richard Odada (AaB, Denmark), Teddy Akumu (Sagan Tosu, Japan), Kenneth Muguna (Kenya Police), Timothy Ouma (IF Elfsborg, Sweden), Duke Abuya (Singida Fountain Gate, Tanzania), Ayub Masika (Nanjing City Football Club, China), Alfred Scriven (IL Hødd, Norway), Clarke Oduor (Bradford City AFC, England).

Washambulizi

Moses Shummah (Kakamega Homeboyz), Elvis Rupia (Kenya Police), Michael Olunga (Al Duhail, Qatar), Masud Juma (Al Jabalain, Saudi Arabia).

Share This Article