Timu ya taifa ya soka ya Kenya, Harambee Stars, imeshuka kwa nafasi mbili kwenye msimamo wa Dunia FIFA wa mwezi huu uliotolewa leo.
Kenya ni ya 112 mwezi Septemba kutoka nafasi ya 110 iliyokuwa ikishikilia mwezi Agosti.
Harambee Stars imeshuka baada ya kushindwa na Gambia kwa mabao 3-1, katika mechi ya kundi F kufuzu kwa Kombe la Dunia mapema mwezi huu.
Uganda ni ya kwanza Afrika Mashariki, ikishikilia nafasi ya 82 kati ya 84 ya mwezi jana, ikifuatwa na Tanzania katika nafasi ya 117.
Morocco ingali ya kwanza Afrika ikiwa ya 13, ikifuatwa na Senegal katika nafasi ya 18 huku Misri ikiwa ya 35.
Uhispania imechupa hadi nafasi ya kwanza ikifuatwa na Ufaransa huku mabingwa wa Dunia Argentina wakishuka hadi nafasi ya tatu.