Harambee Stars yapiga mazoezi ya kwanza Zanzibar tayari kwa Mapinduzi Cup

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya Kenya ya soka ,Harambee Stars imefanya mazoezi ya kwanza Alhamisi jioni baada ya kuwasili kisiwani Zanzibar kujiandaa kwa mashindano ya kuwania Kombe la Mapinduzi.

Kikosi hicho chjini ya kaimu kocha Francis Kimanzi kitafungua kampeini ya mashindano hayo dhidi ya Burkinafaso Jumamosi hii.

Kenya itarejea uwanjani kwa mchuano wa pili dhidi ya Tanzania Jumanne ijayo kabla ya kuhitimisha ratiba dhidi ya wenyeji Zanzibar Januari 10.

Wachezaji 24 walioteuliwa kwa michuano hiyo ni:-

Makipa:Byrne Odhiambo, Faruk Shikalo, Sepstanious Wekesa.

Mabeki: Sylvester Owino, Hanif Wesonga, Alphonce Omija, Brian Okoth, Abud Omar, Siraj Mohammed, Ronney Onyango, Daniel Sakari.

Viungo: Michael Mutinda, Chrispine Erambo, Brian Musa, Kelly Madada, Austine Odhiambo, Kenneth Muguna, Ben Stanley Omondi, Mohammed Bajaber, Boniface Muchiri, Darius Msagah, James Kinyanjui.
21. Moses Shumah

Washambulizi: Moses Shumah, Ryan Ogam.

Kenya inatumia mashindano hayo kujiandaa kwa dimba la bara Afrika kwa wachezaji wa Ligi za nyumbani maarufu kama CHAN, kitakachoandaliwa kwa pamoja na mataifa ya Kenya,Uganda na Tanzania kati ya tarehe 1 na 28 mwezi ujao.

 

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *