Harambee Stars yakamilisha mazoezi kabla ya safari ya Cameroon

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu taifa ya Soka ya Kenya,Harambee Stars ilikamilisha mazoezi jana jioni katika uwanja wa Police Sacco, kujiandaa kwa mechi ya tatu ya kundi J, kufuzu kwa fainali za kombe la Afrika kesho kutwa dhidi ya Indomitable Lions ya Cameroon.

Kikosi cha Harambee Stars kimepigwa jeki na kurejea kwa mshambulizi  na nahodha Michael Olunga ambaye alikosa mechi za mwezi jana dhidi ya Zimbabwe na Namibia.

Upande mwingine Kenya chini ya ukufunzi wa Egin Firat atakosa huduma za kiungo Austin Odhiambo, anayeuguza jeraha la goti na Keneth Muguna.

Mchuano huo utapigwa katika uchanjaa wa Japoma mjini Doula kuanzia saa moja usiku,  huku mechi ya marudio ikisakatwa Jumatatu ijayo Oktoba 11 uwanjani Nelson Mandela jijini Kampala Uganda.

Cameroon na Kenya wanaongoza kundi J kwa pointi 4 kila moja .

Timu mbili bora baada ya kukamilika kwa mechi za kufuzu mwezi ujao zitafuzu kushiriki kipute cha AFCON kati ya Disemba mwaka 2025 na Januari mwaka 2026 nchini Morocco.

 

Share This Article