Harambee Stars yainyofoa Grenada 3-0, yamaliza ya tatu mashindano ya FIFA Series

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars imeikomoa Grenada magoli matatu kwa nunge katika mchuano wa kirafiki maarufu kama FIFA Series, uliosakatwa Jumatatu jioni katika uwanja wa Amahoro mjini Kigali, Rwanda.

Austin Odiambo alifungua ukurasa wa magoli kwa vijana wa Benni McCarthy kunako dakika ya 13 kabla ya Ryan Ogam kutanua uongozi  wa Kenya katika dakika ya 18.

Kenya walirejea kipindi cha pili wakiwa legelege lakini wakabahatika kupata goli la tatu dakika ya 81, baada ya Vijay Valcin wa Grenada kujifunga.

Stars walicheza mchuano huo baada ya kushindwa kwenye nusu fainali na Estonia kupitia penalti wiki iliyopita.

Share This Article