Harambee Stars yaelekea Afrika Kusini

Kenya inatumia michuano hiyo kujiandaa kwa mechi za mbili za ufunguzi kufuzu kwa fainali za AFCON, Septemba mwaka huu dhidi ya Guinea na Eritrea.

Dismas Otuke
0 Min Read

Timu ya soka ya Kenya ya wanaume imeondoka nchini mapema Jumanne kuelekea Pretoria,Afrika Kusini, kucheza mechi mbili za kujinoa makali.

Harambee Stars inayoongozwa na Benni McCarthy, imeratibiwa kuchuana na Lesotho, katika michuano miwili ya kirafiki Juni 4 na 7 mjini Pretoria.

Kenya inatumia michuano hiyo kujiandaa kwa mechi za mbili za ufunguzi za kufuzu kwa fainali za AFCON, Septemba mwaka huu dhidi ya Guinea na Eritrea.

Share This Article