China kuwapeleka matabibu DRC kukabiliana na Ebola

Tom Mathinji
1 Min Read

Huku ugonjwa wa Ebola ukiendelea kuibua wasiwasi wa kiafya katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na mataifa jirani, Tume ya Kitaifa ya Afya ya China (NHC) imesema itapeleka wataalam kusaidia kukabiliana na ugonjwa huo.

Kulingana na tume hiyo, kundi la wataalamu wa matibabu wa China limeondoka jijini Beijing mapema leo Jumanne kuelekea DRC kwa lengo la kuunga mkono juhudi za nchi hiyo za kudhibiti mlipuko wa Ebola.

Hatua hiyo ya serikali ya China imjiri baada ya Shirika la Afya Duniani (WHO)  kutangaza mlipuko wa ugonjwa huo nchini DRC kuwa dharura ya afya ya umma kimataifa.

Madaktari hao wanatarajiwa kushirikiana na timu ya madaktari wa China ambao tayari wako  nchini DRC kudhibiti msambao wa ugonjwa huo.

Ugonjwa wa Ebola ulilipuka katika eneo la Ituri Kaskazini mwa DRC, na umeenea hadi nchini Uganda ambako visa tisa vimethibitishwa.

TAGGED:
Share This Article