Harambee Stars yaangukia Ivory Coast safari ya Kombe la Dunia mwaka 2026

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa Harambee Stars imepangwa kundi gumu la G pamoja na Ivory Coast, Gabon, Burundi, Gambia na Ushelisheli katika mechi za kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia mwaka 2026.

Hii ni kulingana na droo iliyoandaliwa jana Alhamisi jijini Abidjan nchini Ivory Coast, wakati wa kikao cha 45 cha Shirikisho la Soka barani Afrika kilichoongozwa na Kinrara wa CAF Dkt. Patrice Motsepe.

Mataifa 54 yalitengwa katika makundi 9 ya timu 6 kila moja.

Mechi hizo zitang’oa nanga Novemba mwaka huu huku timu bora kutoka kila kundi, baada ya michuano 10, zikifuzu kwenda Kombe la Dunia.

Timu nne bora katika nafasi za pili zitacheza mchujo wa kutafuta timu moja itakayocheza mchujo wa baina ya mabara.

Kipute cha Kombe la Dunia mwaka 2026 kitaandaliwa katika mataifa ya Marekani, Canada na Mexico.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *