Harambee Stars wanoa makali  kabla ya kukwea mchongoma nchini  Ivory Coast

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya soka ya Kenya, Harambee Stars, imefanya mazoezi ya mwisho leo kujindaa kwa mchuano wa mwisho wa kundi F kufuzu kwa Kombe la Dunia dhidi ya wenyeji Ivory Coast kesho usiku.

Kenya, iliyo ya nne kundini kwa alama 12, itakabiliana na mabingwa wa Afrika katika uwanja wa Allasane Ouattara mjini Abidjan kuanzia saa nne usiku.

Pambano hilo ni muhimu kwa wenyeji wanaohitaji tu ushindi ili kufuzu kwa Kombe la Dunia mwaka ujao.

Aidha, Harambee Stars wanahitaji sare au ushindi ili kujiongezea alama kwenye msimamo wa dunia.

Timu zote zilitoka sare tasa kwenye duru ya kwanza iliyopigwa nchini Malawi Juni 11 mwaka uliopita.

Website |  + posts
Share This Article