Timu ya taifa ya Kenya-Harambee Stars ilipoteza bao moja kwa nunge katika mechi ya kimataifa ya kirafiki iliyochezwa Jumapili Alasiri katika uchanjaa wa National Sports Complex of the Côte d’Or nchini Mauritius.
Wenyeji walipachika bao pekee na la ushindi kunako dakika ya 26 kupitia kwa kiungo Kengy Saramandif kufuatia makosa ya mabeki wa Harambee Stars kushindwa kuondosha mpira katika lango lao.
Kenya chini ya ukufunzi wa Engin Firat walijaribu kurejea mchezoni lakini walikosa kumakinika na kuambulia kichapo.
Mauritius walitwaa taji ya michuano hiyo ya kirafiki iliyoshirikisha mataifa manne yakiwemo Pakistan na Djibouti.