Timu ya Harambee Stars, itashuka katika uwanja wa kitaifa wa Nyayo, kesho alasiri kuanzia saa kumi kwa mechi ya mzunguko wa sita kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia mwaka ujao.
Harambee Stars watakabiliana na Pathers ya Gabon, wakilenga kulipiza kisasi cha kushindwa mabao 2-1 novemba mwaka 2023 katika duru ya kwanza mjini Franceville.
Hata hivyo, Kenya inasalia na fursa finyu ya kufuzu kwa Kombe la Dunia baada ya kusajili ushindi mmoja kutoka sare tatu na kupoteza mechi moja kati ya sita walizocheza.
Harambee Stars chini ya kocha Benni McCarthy, inasalia ya tatu kwa alama 6, nyuma ya mabingwa wa Afrika, Ivory Coast, walio na alama 13, pointi moja nyuma ya Gabon.
Burundi ni ya tatu kwa alama 7, Gambia wa pointi 4 huku Ushelisheli ikibura mkia bila alama.
Kenya ni sharti washinde mechi zote tatu zilizosalia ili kuwa na fursa ya kufuzu kwa kombe la dunia mwaka ujao.
Mechi hizo tatu za tatu za Kenya ni itakapowaalika Gabon kesho, kuwaalika Gambia na Ushelisheli mwezi Septemba na kukamilisha ratiba ugenini dhidi ya Ivory Coast Nobeba mwaka huu.