Timu ya taifa ya soka ya Kenya, Harambee Stars, itajaribu kujiondolea fedheha ya kuchapwa na Gambia, itakawapoaalika Ushelisheli katika uwanja wa Kasarani leo kuanzia saa kumi alasiri.
Mechi hiyo ya kundi F kufuzu kwa Kombe la Dunia ni ya kuheshimu tu ratiba, timu zote zikiwa tayari ziko nje ya kufuzu.
Harambee Stars walishindwa mabao 3-1 na Gambia, Ijumaa iliyopita katika mechi iliyokatiza fursa ya Kenya kumaliza katika nafasi ya pili ili kucheza mechi za mchujo.
Kenya ina alama 6 katika nafasi ya tano baada ya kushindwa mechi tatu, kutoka sare tatu na kushinda moja.