Harambee Starlets yaelekea Ivory Coast, kujiandaa kwa WAFCON

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya soka ya wanawake ya Kenya imesafiri kuelekea nchini Ivory Coast, mapema Jumamosi kucheza mechi mbili za kujinoa makali kujiandaa kwa kipute cha bara Afrika (WAFCON).

Kenya chini ya ukufunzi wa Beldine Odemba itachuana na Benin katika mchuano wa kwanza wa kirafiki Machi 2 katika uwanja wa Allasane Quattara mjini Abidjan, kabla ya kupimana nguvu na wenyeji siku mbili baadaye.

Haraambee Starlets baadaye wataelekea mjini Miramas, Marseille, Ufaransa, kwa kambi ya mazoezi hadi tarehe 15 mwezi ujao watakapoelekea Morocco kwa WAFCON.

Kenya inayoshiriki WAFCON kwa mara ya pili imejumuishwa kundi A pamoja na wenyeji Morocco,Senegal na Algeria, huku wakifungua dimba dhidi ya Morocco Machi 17.

Share This Article