Uongozi wa kundi la Hamas, umesema umekubali masharti ya makubaliano ya kusitisha mapigano huko Gaza yaliyotolewa na Israel.
Kundi hilo linasema limewafahamisha wapatanishi wa Qatar na Misri kuhusu uamuzi huo.
Katika taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti yake rasmi, Hamas inasema kiongozi wake, Ismail Haniyeh, alifanya mazungumzo kwa njia ya simu na Waziri Mkuu wa Qatar, Sheikh Mohammed bin Abdulrahman Al Thani, na Waziri wa Ujasusi wa Misri, Abbas Kamel, na kuwafahamisha kuhusu uamuzi wa Hamas wa kukubali pendekezo lao kuhusu makubaliano ya kusitisha mapigano.
Maelezo zaidi kuhusiana na uamuzi huo bado hayajatatolewa, ikiwa ni pamoja na mapigano yatasitishwa kwa muda gani na hatma ya mateka wanaozuiliwa huko Gaza.