Hali ya Zack Orji yaendelea kuimarika

Marion Bosire
1 Min Read

Hali ya kiafya ya mwigizaji Zack Orji inazidi kuimarika kulingana na ripoti za hivi punde zaidi.

Orji mwigizaji wa filamu za Nigeria almaarufu Nollywood anasemekana kuzirai akiwa kwenye bafu kabla ya kukimbizwa hospitalini jijini Abuja nchini Nigeria.

Alikuwa amepoteza fahamu alipolazwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi na baada ya muda zikarejea ila hakuweza kuzungumza.

Sasa mwigizaji huyo mkongwe anasemekana kurejelea hali nzuri kwani sasa anaweza hata kuzungumza lakini bado yuko hospitalini.

Wiki kadhaa zilizopita mwigizaji huyo alipelekwa hospitalini baada ya kulalamikia uchovu na maumivu mwilini.

Orji wa umri wa miaka 64 sasa, amekuwa akiigiza kwenye filamu za Nollywood tangu mwaka 1991.

Share This Article