Hakuna migawanyiko serikalini, asema Gachagua

Tom Mathinji
1 Min Read
Naibu Rais Rigathi Gachagua.

Naibu Rais Rigathi Gachagua amepuuzilia mbali madai kwamba kuna  malumbano katika utawala wa Kenya Kwanza, akisema kuwa serikali inafanya kazi kwa Umoja kutimiza ahadi kwa wakenya.

Gachagua alisema ni wajibu wake kuhakikisha Kuna nidhamu miongoni mwa maafisa wa serikali.

Juma lililopita, naibu huyo wa Rais aliwataka watumishibwa ummakuwahutubia wakenya kwa heshima na unyenyekevu.

Matamshi ya Gachagua yalijiri baada ya Waziri wa biashara na uwekezaji Moses Kuria kuwahutubia wakenya kwa njia iliyotajwa kuwa isiyokuwa na heshima.

Kutokana mwongozo wa Gachagua, madai yaliibuliwa kuwa Kuna migawanyiko serikalini.

“Nilikuwa tu nikitoa mwongozo kwa Waziri Kuria kuhusu jinsi ya kuwaslliana. Hakuna wakati ambapo Naibu Rais atalumbana na wanaofanya kazi chini yake,” alisema Gachagua..

Aidha Gachagua alisema hakuna mabadiliko yatafanywa katika baraza la mawaziri.

Aliwaonya wale wanaojaribu kusambaratisha serikali kuwa hawatafaulu.

Share This Article